1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

F1: Vettel aibuka mshindi Hungary

31 Julai 2017

Mjerumani Sebastian Vettel wa timu ya Ferrari ameupanua uongozi wake katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa dunia baada ya kushinda mbio za Jumapili za Grand Prix nchini Hungary

https://p.dw.com/p/2hS3f
Formel 1- Großer Preis von Ungarn- Sebastian Vettel feiert Sieg
Picha: Reuters/L. Balogh

Vettel, bingwa mara nne wa dunia sasa anaongoza msimamo wa ubingwa wa madereva akiwa na pengo la pointi 14 mbele ya nambari mbili Hamilton. Msikilize Vettel "Nna furaha kubwa. Yalikuwa mashindano magumu, labda hayakuonekana hivyo lakini nilikuwa na mengi ya kufanya. Kulikuwa na hitilafu, sijui ni kwa nini usukani ulianza kwenda kila upande na ukaonekana kuharibika hata zaidi. Lakini nilijitahidi ili kuliweka vizuri gari langu. Haikuwa rahisi. Lakini ilinibidi niwe makindi katika muda wote wa mashindao.

Dereva mwingine wa Ferrari Kimi Raikonnen alipanda jukwaani katika nafasi ya pili baada ya kupewa maagizo na timu yake asimpiku Vettel.

Bingwa mara tatu Hamilton, aliruhusiwa na timu yake kumpiku mwenzake wa Mercedes Valtteri Bottas na kukamata nafasi ya tatu ili ajaribu kupambana na Raikonnen. Lakini Raikonnen alikaa ngangari na hakumpa nafasi Hamilton, kisha Muingereza huyo akamamua kumrudishia nafasi ya tatu mwenzake Bottas katika mzunguko wa mwisho, wakati alipunguza kasi na Bottas akamaliza wa tatu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri:Yusuf Saumu