1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fukushima, hatari ya kuyeyuka nyuklia ingalipo nchini Japan

Abdu Said Mtullya27 Machi 2011

Hatari ya kuyeyuka nyuklia kwenye kinu nambari 2 bado ni kubwa nchini Japan.

https://p.dw.com/p/10iAL
Wafanyakazi wakijaribu kukirekebisha kinu cha nyuklia,nchini JapanPicha: AP

Kiwango cha mionzi kimeongezeka kwenye kinu cha nyuklia nambari 2 cha Fukushima nchini Japan.

Kwa mujibu wa wahusika kiwango hicho kimevuka kile cha kawaida mara milioni kumi.Wafanyakazi waliokuwa wanajaribu kukirebisha kinu hicho kilichoharibika sana baada ya kukumbwa na maafa wamelazimika kuondolewa na kupelekwa kwenye sehemu salama.

Kampuni inayokiendesha kinu hicho, ya Tokyo Electric, TEPCO imearifu kuwa maji yalioingia mionzi yamo chini ya injini iliyopo katika jengo lililounganishwa na kinu hicho nambari 2.Kinu hicho kilichopo Fukushima kiliharibiwa vibaya kutokana na mitetemeko ya ardhi na Tsunami wiki mbili zilizopita.Kampuni ya TEPCO imejaribu kuyaondoa maji yaliyoingia mionzi ya nyuklia kwenye vinu vinne vya Fukushima.

Wakati huo huo mashirika ya habari yamearifu kuwa hatari ya kutokea maafa makubwa ya kuyeyuka kwa nyuklia bado ingalipo.