1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G20 yaunga mkono juhudi za kupambana na upotoshaji

14 Septemba 2024

Mawaziri wa mataifa ya G20 wanaokutana Brazil wameunga mkono juhudi za kupambana na upotoshaji na kuunda ajenda kuhusu akili mnemba.

https://p.dw.com/p/4kcVz
Mkutano wa G20 wa Brazil huko Rio de Janeiro | Mauro Vieira
Mawaziri wa G20 wameunga mkono juhudi za kukabilana na upotoshaji na akili mnemba.Picha: Mauro Pimentel/AFP/Getty Images

Viongozi wa kundi la mataifa 20 yaliostawi na yanayoinukia kiuchumi wamekubaliana jana IJumaa kujiunga na juhudi za kupambana na taarifa za upotoshaji na kuunda ajenda kuhusu akili mnemba, mnamo wakati serikali zao zikipambana dhidi ya kasi, ukubwa na ueneaji wa upotoshaji na matamshi ya chuki.

Mawaziri hao waliokutuna wiki hii katika mji wa Maceio nchini Brazil, walisisitiza katika taarifa juu ya haja ya majukwa ya kidijitali kuonesha uwazi na kufuata sera muhimu na mifumo ya kisheria.

Ni mara ya kwanza katika historia ya G20, kwamba kundi hilo limetambua tatizo ya taarifa za upotoshaji na kutoa wito wa uwazi na uwajibikaji kutoka majukwaa ya kidijitali.

Wawakilishi wa G20 pia walikubaliana kuanzisha miongozo ya uendelezaji wa akili mnemba, na kutoa wito wa matumizi ya kimaadili, wazi na ya uwajibikaji ya akili mnemba.