G7 kuisaidia Ukraine kwa kutumia mali za Urusi ilizozizuia
25 Mei 2024Matangazo
Wakuu wa taasisi za kifedha wa kundi hilo wamesema hayo hii leo, hii ikiwa ni kulingana na rasimu ya taarifa ambayo shirika la habari la Reuters limepata nakala yake.
Kundi la G7 limezuia mali za Urusi zenye thamani ya dola bilioni 300 , muda mfupi baada ya kuivamia Ukraine, Februari 2022.
Duru kutoka kwenye kundi hilo zimesema rasimu hiyo haitafanyiwa marekebisho makubwa kabla ya toleo la mwisho kutangazwa rasmi baade hii leo.