Ghana yapata makubaliano ya kuangalia upya deni lake
24 Mei 2024Matangazo
Waziri wa Fedha wa Ghana, Mohammed Amin Adam, amesema wataudurusu kwa haraka mkataba huo kwa lengo la kuusaini.
Mkataba huo unasafisha njia kwa bodi ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kukutana wiki ijayo kuidhinisha mkopo wa milioni 360 utakaotolewa chini ya mpango maalum wa kuikwamuwa kiuchumi nchi hiyo wa dola bilioni 3.
Soma zaidi: Je mkutano wa G8 utatoa matumaini kwa Afrika?
Mnamo Disemba2022, Ghana ilishindwa kulipa deni lake la nje baada ya gharama za huduma kupanda na kuwa nchi ya pili ya Afrika, baada ya Zambia, kushindwa kusimamia madeni yake wakati wa janga la UVIKO-19.