Afrika yatakiwa kuungana kuhusu fidia ya biashara ya utumwa
15 Novemba 2023Baadhi ya viongozi wa Magharibi katika siku za karibuni wamekiri maovu yaliyofanywa wakati wa enzi ya ukoloni Afrika na majumba ya makumbusho yameanza kurejesha mali zilizoibwa na kazi za sanaa.
Lakini dhana ya kulipa fidia ya kifedha kuhusu biashara ya mamilioni ya watumwa waliosafirishwa kutoka Afrika Magharibi na Afrika ya Kati bado halieleweki.
Ghana kuzingatia nidhamu kuhusu mkopo wa IMF
Akufo-Addo amesema katika kongamano la viongozi wa Afrika la kujadili masuala ya fidia mjini Accra kuwa hakuna kiasi cha fedha kinachoweza kurekebisha uharibifu uliosababishwa na biashara ya utumwa na madhara yaliyofuatia.
Lakini, hilo ni suala ambalo ulimwengu lazima ulikabili na hauwezi kulipuuza. Amesema hata kabla ya kukamilika mazungumzo ya fidia, bara zima la Afrika linastahili kuombwa radhi rasmi kutoka kwa mataifa ya Ulaya yaliyohusika na biashara ya utumwa.