1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres ataka mkutano wa COP28 utumike kuinusuru dunia

28 Novemba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewatolea mwito viongozi kuutumia mkutano ujao wa mazingira wa COP28 kukomesha ongezeko la joto ulimwenguni na kuyeyuka kwa theluji kwenye ncha mbili za sayari

https://p.dw.com/p/4ZVYI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Brendan McDermid/REUTERS

Akizungumza na waandishi habari mjini New York kuelekea mkutano wa COP28 utakaofanyika huko Dubai, Guterres amesema viongozi ni lazima wachukue hatua sasa kupunguza kiwango cha joto kupindukia nyuzi 1.5 za Celcius.

Amewataka vilevile watumie nafasi ya mkutano huo unaoanza siku ya Alhamisi kuwalinda watu dhidi ya balaa inayokanayo na mabadiliko ya tabianchi na kufikia uamuzi wa kuachana na enzi ya kutumia nishati za visukuku.

Guterres ambaye hivi karibuni alikuwa ziarani kwenye bara la Antarctica amesema kasi ya kuyeyuka kwa barafu kwenye ncha mbili za dunia kunachangia kupanda kwa kina cha bahari na pia kuongeza joto kwenye uso wa dunia.