1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Athari za mabadiliko ya tabia nchi ni kubwa

7 Novemba 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametahadharisha kwamba dunia haiko tayari kwa "janga" litakalosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na inastahili kujiandaa kwa mikasa mibaya zaidi katika siku zijazo.

https://p.dw.com/p/4mkye
Athari za mafuriko nchini Uhispania
Athari za mafuriko nchini UhispaniaPicha: Bruna Casas/REUTERS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametahadharisha kwamba dunia haiko tayari kwa "janga" litakalosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na inastahili kujiandaa kwa mikasa mibaya zaidi katika siku zijazo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kila mwaka ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP kuhusu pengo lililopo katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, Guterres amesema kwa sasa athari za mabadiliko hayo zinaonekana katika kila pembe ya dunia na hakuna nchi ambayo ina kinga ya hilo.

Soma: Nchi tajiri zalaumiwa kwa kitisho cha kimazingira

Mataifa tajiri duniani yako kwenye shinikizo katika mkutano wa kilele wa COP29 mwezi huu, kuongeza kwa kiasi kikubwa ahadi yao ya dola bilioni 100 kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabi nchi katika nchi zinazoinukia kiuchumi.