1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gutteres: Lebanon iko kwenye ukingo wa vita kamili

24 Septemba 2024

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amewaonya leo viongozi wa dunia kwamba Lebanon iko kwenye ukingo wa kutumbukia kwenye vita kamili huku mapigano yakiongezeka kati ya Israel na kundi la Hezbollah.

https://p.dw.com/p/4l2ab
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Richard Drew/AP Photo/picture alliance

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amewaonya leo viongozi wa dunia kwamba Lebanon iko kwenye ukingo wa kutumbukia kwenye vita kamili huku mapigano yakiongezeka kati ya Israel na kundi la Hezbollah.

Akihutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, Guterres amesema kwamba viongozi wote wanapaswa kushtushwa na ongezeko hilo la mapigano na kuonya dhidi ya uwezekano wa kuibadilisha Lebanon kuwa Gaza nyingine huku akiitaja hali katika eneo hilo kama jinamizi lisilokoma.

Soma: Viongozi wa dunia kuhutubia Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa

Katika mkutano huo wa kilele wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Marekani Joe Biden  amesema uvamizi wa Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini Ukraine umeshindwa na akatoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuendelea kuiunga mkono Ukraine hadi itakapopata ushindi.Rais Biden pia amewatoa mwito wa kumalizwa vita vya Gaza na Sudan. Biden alihutubia mkutano huo kwa mara ya mwisho kama Rais wa Marekani.