1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ngumu Lysychansk Ukraine

27 Juni 2022

Nchini Ukraine tawala za mikoa huko mashariki ya Ukraine leo hii zimetaka kuondolewa kwa dharura raia katika mji wa Lysychansk ambao kwa sasa unashambuliwa vikali na vikosi vya Urusi,

https://p.dw.com/p/4DIb0
Russlands Angriff auf die Ukraine geht weiter, in Lysychansk
Picha: Oleksandr Ratushniak/REUTERS

Hayo yanaendelea huku ripoti zinasema kwa mara ya kwanza ndani ya siku 22 za mwanzo za Juni usafirishaji wa nafaka nje ya taifa hilo umeporomoka kwa asilimia 40.

Kupitia ukurasa wake wa telegram Gavana wa Lysychansk, Serhiy Gaidai amesema wakazi wa eneo hilo, ndugu na jamaa, kutokana na uwepo wa kitisho halisi cha uhai na afya wanatoa wito wa kujinusuru kwa haraka sana. Gavana huyo anasema hali ilivyo katika mji huo ni mbaya sana, ingwa hajasema hadi sasa watu wangapi wamesalia katika eneo hilo. Lakini kimsingi rekodi zinaonesha kiasi ya watu laki moja wamekuwa wakiishi hapo kabla ya uvamizi wa Urusi wa Februari 24.

Mji wa Lysychansk  waripotiwa kuwa katika hali ya janga.

Ukraine | Zerstörung in Lyssytschansk
Athari za makombora ya Urusi LysychanskPicha: Anatolii Stepanov/AFP

Hapo awali kabisa gavana Gaidai alisema mji wa Lysychansk upo katika hali ya janga kutokana na mashambulizi ya makombora ya Urusi yanayoulenga mji huo. Anasema kumekuwa kuwa uharibifu mkubwa, baada ya vikosi vya Urusi mwishoni wa juma kufanikiwa kuudhibiti mji mwinginwa jirani wa Sievierodonetsk.

Kwa zingatio la duru za kijeshi katika mji huohuo wa kimkakati wa Lysychansk, kunaelezwa kuwa jeshi limefanikiwa kuzuia jitihada ya kuuzingira mji huo ya jeshi la Urusi. Ofisi ya mkuu wa majeshi wa Ukraine imesema  katika eneo jirani la Verkhnyokamyanka jeshi la Ukraine limewashambulia vikali wale wa Urusi na kuwafanya wasalimu amri. Eneo hilo lipo karibu na barabara muhimu, umbali wa kilometa chache kutoka Lysychansk.

Miji ya Bachmut, Kherson na Odessa mapigano yanaendelea.

Lakini pia mapigano yanendelea katika eneo la mbali la msahraiki la mkoa wa Bachmut, pamoja na mwingine wa Kherson uliopo katika ukanda wa Bahari Nyeusi. Sehemu nyingine, mji wa Odessa kusini mwa Ukraine makombora ya Urusi yamesababisha athari kwa watu sita akiwemo mtoto mmoja. Kamandi ya kijeshi ya Ukraine katika eneo hilo imesema vikosi vya Urusi vilifyatua bomu aina ya Tu-22. Hata hivyo haijaweza kufahamika mara moja kwa tukio hilo mamlaka imetangaza majeruhi au vifo.

Kwa ujumla nchini Ukraine kumeripotiwa ongezeko la mashambulizi ya Urusi kutoka pande tofaut tangu mwishoni mwa juma. Mashambulizi yote hayo yanaelezwa kuvuka mpaka wa maeneo ya uwanja wa vita.

Soma zaidi;G7 yaweka hazina ya miundombinu kwa nchi zinazostawi

katika suala za mazao ya kilimo, Wizara ya Kilimo imesema mauzo ya nje katika siku 22 za kwanza za Juni yamepungua kwa karibu asilimia 44 ikiwa sawa na tani milioni 1.11 kwa mwaka uliopita. Kiasi hicho kilijumuisha tani 978,000 za mahindi, tani 104,000.

ya ngano na tani 24,000 za shayiri.

Kwa kawaida Ukraine kabla ya uvamizi wa Urusi Ukraine inasafrisha tani milioni 6 za nafaska kila mwezi.

Vyanzo: DPA/RTR