Hali ni mbaya kwenye vituo vya karantini, Kenya
28 Mei 2020Serikali ya Kenya imelaumiwa kuhusiana na jinsi inavyokabiliana na ugonjwa wa Covid-19.
Tokea katikati mwa mwezi Machi,serikali ya Kenya imewaweka karantini ya siku 14 watu wanaoingia nchini humo au wale waliotangamana moja kwa moja na wagonjwa na vileile wale wanaotokea kwenye kaunti ambazo hakukueko na amri ya kutotoka nje.
Walio na uwezo walijiweka karantini kwenye hoteli za kifahari na wengine walipelekwa kwenye vituo vilivyoandaliwa na serikali katika baadhi ya shule na vyuo vikuu.
Maandamano yalizuka kweye baadhi ya vituo na wengine kutoroka vituo vya karantini. Kesi mbili zinaikabili serikali kuhusu tuhuma za mateso waliofanyiwa watu waliowekwa karantini, serikali bado haijajibu tuhuma hizo.
Shirika la habari la Reuters liliwahoji watu 12 waliowekwa kwenye karantini,wawili walielezea kwamba mazingira yalikuwa ya kuridhisha,lakini 10 ambao walikataa kutajwa majina yao kwa hofu ya kunyanyapaliwa wamesema kwamba vituo hivyo ni chakavu,wakielezea kwamba vitanda vimekuwa na kunguni, na pia choo na chakula vibaya.
Shirika la Reuters lilitaka kupata maoni ya viongozi wa vituo hivyo lakini simu na ujumbe wa simu waliotumiwa viongozi hao havikupata majibu kwa wiki kadhaa. Judy sirima msemaji wa wizara ya afya alikataa kuzungumza.
Mwanamke mmoja ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba aliwekwa karantini kwenye chuo cha mafunzo ya matibabu cha Nairobi kwa wiki mbili na baadae uchunguzi ukaonyesha kwamba hana virusi vya Corona. Watu wengine waliambukizwa katika vituo ambavyo vilishuhudia misongamano ya watu wakati wa kugawa chakula, na mwanamke huyo pia baada ya wiki nyingine moja alijikuta ameambukizwa na virusi.
Niliambukizwa kutokana na karantini kwa sababu tulikuwa tukitumia choo kimoja,alisema. Lakini shirika la Reuters halikuweza kuthibitisha mahala alipoambukizwa virusi vya Corona.
Mwanamke mwengine kwenye kituo cha Karen Cooperative Retreat and Conference Center alikowekwa karantini na watu wengine amesema kwamba hawakupewa glavu,barakoa au vitakatishi.
Vituo vyote hivyo havikutaka kutoa maoni.
Tayari Kenya ,taifa lenye wakaazi milioni 47 ,imerekodi visa 1348 vikiwemo vifo 52 vya ugonjwa wa Covid-19 na kutokana na ukosefu wa vifaa ni mwezi huu ndio ilianzisha vipimo kwa idadi kubwa ya watu. Wizara ya afya ilisema Jumapili kwenye mtandao wake wa twitter kwamba watu wengi waliofanyiwa vipimo walidanganya kuhusu anuani zao.
Robert Alai,anayeongoza mtandao wa kujitegemea hakusita kujibu kwa ujumbe huo wa wizara ya Afya na kusema kwamba inaeleweka watu kufanya hivyo,kwa sababu watu waliowekwa karantini wahudumiwa kama nguruwe.
Ripoti ya bunge la seneti mwezi uliopita ilieleza kwamba mamia ya watu waliokiuka amri ya kutotoka nje walishikiliwa na kuwekwa kwenye vituo sawa na washukiwa wa virusi vya corona.
Mashirika: Reuters