Hali sasa ni tulivu nchini Guinea
30 Septemba 2009Matangazo
Viongozi wa upinzani wamekula kiapo kuendelea na maandamano ya kuupinga utawala wa kijeshi wa
Kapteni Moussa Dadis Camara, baada ya watu 157 kuuawa pale wanajeshi walipofyatua risasi
dhidi ya waandamanaji Jumatatu iliopita. Maandamano hayo yaliitishwa na wanasiasa wa upinzani
kupinga mpango wa Kiongozi wa kijeshi kutaka kuwa mgombea katika uchaguzi ujao akiwa na
lengo la kubakia madarakani, licha ya kusema wakati alipotwaa madaraka kuwa hakuwa na azma
hiyo. Mohamed AbdulRahman amezungumza na Mwandishi Habari na mchambuzi wa
masuala ya Afrika Jenerali Ulimwengu akiwa Dar es salaam, na kwanza alimuuliza matukio haya
yanaashiria nini katika siasa za Guinea chini ya uongozi wa sasa .
Mtayarishaji: Mohamed Abdulrahman
Mhariri: Othman Miraji