1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya usalama nchini Ujerumani bado ni tete, majasusi

18 Juni 2024

Maafisa nchini Ujerumani wamesema hali ya usalama nchini humo bado ni tete, wakiangazia vitisho vya ndani na nje kutokana na ujasusi na taarifa potofu za itikadi kali.

https://p.dw.com/p/4hCmu
Nancy Faeser (Kulia) waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani asema mamlaka za usalama zimechukua hatua za kila mara za kuzuia mashambulizi yanayoweza kutokea nchini Ujerumani.
Nancy Faeser (Kulia) waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani asema mamlaka za usalama zimechukua hatua za kila mara za kuzuia mashambulizi yanayoweza kutokea nchini Ujerumani.Picha: Axel Schmidt/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser amesema wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya mwaka 2023 kuhusu ulinzi wa katiba kwamba Urusi, China na Iran wamekuwa wakitumia idara za intelijensia kwa kiasi kikubwa kuipeleleza Ujerumani.

"Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani: Urusi, China na Iran hasa wamekuwa wakitumia idara za kijasusi kuipeleleza Ujerumani. Kuna pia majaribio yanayoendelea ya kufuatiliana na kuwaua wapinzani wanaoishi nchini humo. Mamlaka zetu za usalama zimechukua hatua za kila mara za kuzuia mashambulizi yanayoweza kutokea nchini Ujerumani. Tutaendelea kufanya kila tuwezalo kukwamisha mipango hiyo,” amesema Nancy Faeser.

Idara hiyo aidha imesema kulikuwa na ongezeko la visa vya ghasia zilizochochewa na wafuasi wa mrengo wa kulia vilivyofikia 14,500 mwaka 2023 toka 14,000 mwaka 2022.