Hamas lajiondoa kwenye mazungumzo ya usitishaji vita Gaza
14 Julai 2024Afisa huyo ambaye hakutajwa jina ameeleza kuwa, kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh amewaambia wasuluhishi wa kimataifa kuwa uamuzi huo umefanyika kutokana na Israel kutokuwa na nia ya dhati, na kuendelea kuahirisha na kuzuia mazungumzo hayo, pamoja na mauaji yanayoendelea dhidi ya raia wasio na silaha.
Hayo yanajiri wakati Wapalestina wasiopungua 17 wameuwawa baada ya Israel kufanya mashambulizi ya anga katika mji wa Gaza jumapili asubuhi. Maafisa wa afya na huduma za dharura katika eneo hilo wanaodhibitiwa na Hamas wamearifu kuwa, watu wengine 50 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Soma zaidi: Operesheni mpya ya Kijeshi Gaza yakosolewa na UN
Katika hatua nyingine, afisa wa ngazi ya juu wa kundi la Hamas amesema kiongozi wa kijeshi wa kundi hilo Mohammed Deif yuko salama baada ya jaribio la kumuua lililofanywa na jeshi la Israel katika shambulio la anga. Afisa huyo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, Deif anaendelea na shughuli zake za kusimamia operesheni za tawi la kijeshi la Hamas.