Hamas watoa vidio ikionyesha mateka wanaoshikiliwa
28 Aprili 2024Kundi la wanamgambo la Hamas, jana limeachia mkanda wa vidio unaowaonyesha mateka ambao bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza, mnamo wakati maafisa wa Israel na Saudi Arabia wakidokeza uwezekano wa kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano baina ya pande mbili.
Soma: Hamas inatathmini pendekezo jipya la Israel la kusitisha mapigano
Katika mkanda huo wa vidio, mateka wawili walisema kuwa wanaunga mkono makubaliano baina ya Hamas na serikali ya Israel ya kuachiliwa huru mateka wanaoshikiliwa Ukanda wa Gaza.
Mmoja wa mateka katika mkanda huo wa vidio usio na tarehe, alieleza kwamba amekuwa akishikiliwa kwa siku 202. Mateka wa pili, ambaye kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel ana uraia wa Marekani, alitoa wito wa maandamano mjini Tel Aviv na Jerusalem kushinikiza kuachiliwa mateka.
Fuatilia habari hii: Mazungumzo ya kujadili vita vya Gaza kufanyika Saudi Arabia
Jana ilitimia siku ya 204 tangu mauaji ya watu wengi na utekaji kusini mwa Israel mnamo Oktoba 7.