HAMBURG. Chama cha SPD chapendekeza kikomo cha kasi ya magari
28 Oktoba 2007Matangazo
Chama cha Social Democratic, SPD hapa Ujerumani, kinataka kuwekwe kikomo rasmi cha kasi kwa magari yote yanayotumia barabara za hapa nchini, ili kupunguza kiwango cha gesi ya carbon dioxode angani.
Kwenye mkutano wa chama mjini Hamburg, idadi kubwa ya wanachama wa chama cha SPD waliunga mkono pendekezo la mwendo wa kilimota 130 kwa saa kama kikomo rasmi.
Waziri wa mazingira wa Ujerumani, Sigmar Gabriel, anapinga kuweka kikomo cha mwendo, akisema watengenezaji magari hawatakuwa na haja ya kutengeneza injini za magari ambazo hazitakuwa zikichafua mazingira.
Chama cha Christian Democratic Union, CDU, kinapinga pia kuweka kikomo cha kasi katika barabara zote kuu.