Hamburg. Maelfu waandamana wakati wa Pasaka.
28 Machi 2005Matangazo
Zaidi ya watu elfu 10 wameshiriki katika maandamano ya kila mwaka ya wakati wa sikukuu ya pasaka. Maelfu kadha wanatarajiwa kushiriki katika maandamano ya amani mjini Hamburg, Berlin na Frankfurt leo Jumatuta.
Maandamano hayo yanalenga katika kuzishutumu sera za Marekani dhidi ya Iraq pamoja na katiba ya umoja wa Ulaya.
Katika jimbo la mashariki la Brandenburg zaidi ya watu 6,000 wameandamana kupinga dhidi ya eneo la mazoezi ya kijeshi.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Peter Struck anataka eneo la anga la Urusi kulitumia kwa mazoezi ya kutumia silaha.