HAMBURG :Miaka 40 ya uhusiano baina ya Ujerumani na Israel
12 Mei 2005Matangazo
Rais Horst Köhler wa Ujerumani amesifu mahusiano ya kirafiki na mfungamano uliopo baina ya Ujerumani na Israel.
Rais Köhler amesema hayo katika maadhimisho ya mwaka wa 40 tokea nchi mbili hizo zianzishe mahusiano ya kibalozi baina yao.
Bwana Köhler amesema katika makala ya gazeti aliyoandika kwa ajili ya maadhimisho hayo kwamba Ujerumani na Israel zimethibiti kuwa nchi rafiki zinaoweza kuaminiana.
.