Hamburg: Mtuhumiwa wa kushiriki katika kisa cha kuziteka nyara ndege huko Marekani aachwa huru na mahakama ya Ujerumani
9 Juni 2005Mahakama ya rufaa ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani imeihakikisha hukumu ya kutokuwa na hatia iliopitishwa kwa Abdelghani Mzoudi, mwanafunzi wa Kimoroko aliyeshtakiwa kwa kushiriki katika njama ya mashambuluio ya utekaji nyara wa ndege ya Septemba mwaka 2001 huko New York. Mahakama hiyo iliikataa rufaa iliokatwa na waendeshaji mashtaka wa Ujerumani wakiataka kesi hiyo isikilizwe upya na ikahakikisha hukumu ya kumwachia huru iliopitishwa na mahakama ya Hamburg hapo Februari mwaka jana. Bwana Mzoudi anaishi Hamburg na alikuwa rafiki wa mtu aliyeongoza mashambulio ya utekaji nyara ndege, Mohamed Atta, na wanachama wengine wa lile gengi la hamburg.
Hata hivyo, waziri wa mambo ya ndani wa mkoa wa Hamburg, Udo Nagel, amesema atataka Mzoudi afukuzwe kutoka Ujerumani.