Harris na Trump waendelea kujipigia debe kampeni za urais
14 Oktoba 2024Kamala Harris na mpinzani wake Donald Trump waliendeleza kampeni zao katika kinyanganyiro cha urais wakati kura mpya ya maoni ikionyesha kwamba makamu wa rais hana ushawishi wa kutosha miongoni mwa baadhi ya wapiga kura wa jadi wa chama cha Democrats.
Harris alikuwa North Carolina, jimbo lililoathiriwa na kimbunga wiki mbili zilizopita ambacho kilisababisha uharibifu mkubwa na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 235 katika eneo la Kusini-mashariki mwa Marekani.
Soma pia: Kamala Harris amshambulia Trump kwa kumtaja kama tishio kwa uhuru wa wanawake
Katika kampeni yake Trump aliangazia sana suala kuu la uhamiaji katika mkutano wa hadhara huko Arizona, akiahidi katika hotuba yake kwamba ataajiri walinzi wapya 10,000 wa mpaka wa Marekani ikiwa atachaguliwa tena.
Haya yanajiri wakati, polisi ikisema imemkamata mtu mmoja aliyekuwa na bunduki siku ya Jumamosi karibu na eneo la mkutano wa Trump huko California.