Hasara ya nusu mwaka ya Kenya Airways imezidi maradufu
28 Agosti 2019Matangazo
Shirika la ndege la Kenya, ambalo linataifishwa tena kulinusuru kutokana na madeni yanayozidi kulielemea, limeshuhudia hasara yake ya nusu mwaka kabla ya kodi ikiongezeka maradufu kutoka kipidi cha mwaka uliyopita, na kufikia dola milioni 83, kulingana na taarifa yake ya matokeo iliyotolewa jana.
Bunge la Kenya lilipiga kura mwezi Julai kulitaifisha tena shirika hilo linaloendeshwa kwa hasara, na linakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni, na limefanya mabadiliko matatu ya watendaji wakuu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wakati likipambana kushindana na mahasimu wake wa kikanda.
Serikali ya Kenya inapanga kuwarejeshea pesa za wamiliki wa hisa nyingi zaidi likiwemo shirika la Air France-KLM linalomiliki asilmia 7.8 ya hisa.