Hesse, Ujerumani. Waislamu wakamatwa Ujerumani.
29 Septemba 2005Matangazo
Polisi katika jimbo la Hesse nchini Ujerumani wamewakamata watuhumiwa 38 katika matukio kadha yanayolenga Waislamu wenye imani kali.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya jimbo hilo amewaambia waandishi wa habari mjini Wiesbaden kuwa watatu kati ya watuhumiwa hao walikuwa wametayarishiwa hati za kukamatwa wakati watuhumiwa wengine 33 hawakuwa na karatasi muhimu za kuishi nchini Ujerumani.
Msako huo ulifanywa katika miji 20, ikiwa ni pamoja na Frankfurt, siku ya Jumanne. Msako huo ulilenga katika biashara na mashirika yanayotuhumiwa kutafuta fedha kwa ajili ya mashambulizi ya kigaidi.