Hofu Msumbiji kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi
20 Desemba 2024Msumbiji inajiandaa kwa maandamano zaidi pale tangazo la matokeo ya mwisho ya uchaguzi yenye utata litakapotolewa kabla ya siku ya Jumatatu inayokuja.
Kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane ametishia kuitisha vurugu nchi nzima kama Baraza la Kikatiba litaidhinisha matokeo ya awali ambayo yalimuweka katika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa Oktoba 9 akishindwa na mgombea wa chama tawala cha Frelimo.
Soma pia: Mondlane atishia kuanzisha vurugu kubwa Msumbiji
Msumbiji imekumbwa na miezi miwili ya ghasia ambazo zimewauwa watu 130 na kusababisha uharibifu mkubwa. Aidha vurugu hizo za baada ya uchaguzi zimekwamisha shughuli za kibiashara mijini, na kuathiri uzalishaji viwandani.
Serikali ya Marekani jana iliongeza tahadhari yake ikionya dhidi ya safari za kwenda Msumbuji, ikisema maandamano yanaweza kugeuka haraka na kuwa fujo.