Hoja ya uraia pacha yaibuliwa tena visiwani Zanzibar
5 Februari 2024Akichangia mada katika kongamano hilo mwanasiasa mkongwe Hamad Rashid amehoji nafasi ya Zanzibar wakati kiongozi anapotoka nje ya nchi kuwa haimo katika rasimu mpya.
"Zanzibar nafasi yetu ikoje inapokuwa nje ya nchi? "
Soma pia: Mkutano kuhusu uchumi wa Buluu wafanyika visiwani Zanzibar
Miongoni mwa wachangiaji katika mjadala ulofanyika leo mjini Zanzibar na kuwajumuisha wananchi kutoka tasisi mbali mbali za kiraia, serikali na mabalozi wastaafu, wachangiaji wengi wamekumbusha kuwa wakati umefika kwa serikali ya Tanzania kuingiza katika sera uraia pacha na teknolojia ili nchi ifunguke zaidi katika dunia kiuchumi.
"Umefika wakati tuangalia sheria juu ya uraia wa nchi mbili ili kutoa nafasi kwa watu wetu," alisema Rajab Ali.
Tanzania bado haijatumia vya kutosha teknolojia, mitandao na iterneti katika kukuza biashara nchi za nje na kutumia lugha ya Kiswahili na utamaduni kama anavyoeleza katibu tawala mkoa wa kusini, Radhia Khatib Haroub
"Msisitizo mpita wa kulinda utamaduni wa mtanzania na kutumia lugha ya Kiswahili kwani itatoa fursa pana ya utamaduni."
Katibu Mtendaji wa baraza la watu wenye ulemavu Zanzibar, Ussi Khamis Dede amesema licha ya kuwa sera mpya lakini kuna vitu havijazingatia watu wenye ulamavu. "Uzingatiaji wa watu wenye ulemavu bado hakuna kuzingatia kundi la watu wenye ulemavu."
Awali Mwenyekiti wa Kongamano hilo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki, Januari Makamba aliwaambia wana kongamano kwamba sera ya mambo ya nje ni muongozo kushughulikia mahusiano yake na nchi nyengine duniani.
"Hatupo kufanya jambo dogo tupo hapa katika kufanya kazi kubwa ya kutengeneza tamko la taifa ya namna tunawasiliana vipi na dunia."Wahamiaji wapewa uraia visiwani Zanzibar
Baadhi ya Watanzania wanaendelea kujadili rasimu ya mambo ya nje ili kuandika sera mpya ambayo itaendena na mabadiliko duniani, kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye anasema sera ya sasa ya mambo ya nje ya mwaka 2001 imepitwa na wakati.