1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hospitali za Gaza zapungukiwa huduma muhimu

15 Oktoba 2023

Madaktari kwenye Ukanda wa Gaza wametahadharisha kwamba huenda maelfu ya watu wakapoteza maisha ikiwa hospitali zilizojaa watu waliojeruhiwa zitaishiwa mafuta na mahitaji mengine muhimu.

https://p.dw.com/p/4XYJP
Israel, Tel Aviv | Menschen versammeln sich zum Blutspenden nach dem Angriff aus dem Gaza-Streifen
Watu wanajitolea damu mjinin Tel Aviv kwa ajili ya kusaidia majeruhi baada ya shambulizi la GazaPicha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Daktari huyo mkuu katika hospitali ya Ukanda wa Gaza ameeleza kuwa wagonjwa 35 wamelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na wanategemea mashine za kuwasaidia kupumua na wengine 60 wanaofanyiwa huduma ya kusafishwa figo na kwamba mafuta yatakapoisha, watalazimika kuzima mkitambo na hivyo kukatizsha huduma hizo.

Soma zaidi:WHO: Haiwezekani kuwahamisha wagonjwa Gaza

Wakati huohuo raia wanahangaika kutafuta chakula, maji na mahala salama wakati ambapo Israel inajiandaa kufanya operesheni ya ardhini kujibu mashambulio ya Hamas ya wiki iliyopita.