1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Hotuba ya Netanyahu yaibua maandamano mapya Israel

21 Julai 2023

Hotuba iliyotolewa na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ya kutetea mapendekezo yake ya mageuzi tata ya mfumo wa mahakama imeibua maandamano mapya nchini humo.

https://p.dw.com/p/4UEaC
Israel Tel Aviv Proteste gegen Justizreform
Picha: MENAHEM KAHANA/AFP

Kumekuwepo na taarifa za makabiliano kati ya waandamanaji na polisi wakati walipojaribu kufunga barabara kuu mjini Tel Aviv na kuwasha moto, huku watu karibu 1,000 wakiripotiwa kuandamana katika mji wa Jerusalem hii leo. Baadhi ya waandamanaji wamekamatwa, hii ikiwa ni kulingana na gazeti la Haaretz.

Soma pia: Maandamano dhidi ya serikali yatanda Israel

Kwenye hotuba hiyo, Netanyahu alitangaza kwamba muswada huo uliolenga kuimarisha demokrasia huenda ukapitishwa katika siku chache zijazo. Wakosoaji wanasema mabadiliko hayo yanaitia hatarini demokrasia.

Bunge zima la Israel linatarajia kuanza kuupigia kura muswada huo siku ya Jumapili, ingawa haijajulikani wakati utakapoanza kutekelezwa kikamilifu.