1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

HRW lasema makundi ya kujihami yawalenga raia Mali

3 Novemba 2023

Makundi ya wanamgambo wa kiislamu na na wanajeshi wa Mali waliwauwa karibu raia 175, wengi wao wakiwa watoto kati ya mwezi Aprili na Septemba nchini Mali.

https://p.dw.com/p/4YLx4
Human Rights Watch imesema kundi lililo na mafungamano na Al-Qaeda la Support Group for Islam and Muslims GSIM lilihusika na vifo vya karibu watu 135.
Human Rights Watch imesema kundi lililo na mafungamano na Al-Qaeda la Support Group for Islam and Muslims GSIM lilihusika na vifo vya karibu watu 135.Picha: Souleymane Ag Anara/AFP

Hayo yamesemwa na shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch lililoyataja mauaji hayo kama uhalifu wa kivita.

Katika ripoti iliyoonekana na shirika la habari la Ufaransa AFP, Human Rights Watch imesema kundi lililo na mafungamano na Al-Qaeda la Support Group for Islam and Muslims GSIM lilihusika na vifo vya karibu watu 135.

Shirika hilo limelilaumu kundi la GSIM kwa mauaji ya Septemba 7 ya watu 120 yaliyotokea katika feri moja huko Timbuktu.

Shirika hilo limeongeza kwamba wanajeshi wa Mali na wapiganaji kutoka kundi la mamluki wa Urusi la Wagner waliwauwa raia 40 katika operesheni tatu tofauti kati ya Aprili na Septemba.

Watawala wa kijeshi wa Mali waliingia katika ushirikiano na Wagner baada ya majeshi ya Ufaransa kuondoka nchini humo mwaka jana.