1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Tanzania yawafurusha maelfu ya Wamaasai

31 Julai 2024

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, limesema kuwa Tanzania inawafurusha maelfu ya Wamaasai kutoka katika ardhi ya mababu zao.

https://p.dw.com/p/4iyRV
HRW: Tanzania yawafurusha maelfu ya Wamaasai
HRW: Tanzania yawafurusha maelfu ya WamaasaiPicha: Bildagentur-online/Nilsen-McPhoto/picture alliance

Katika ripoti yake iliyotolewa leo, Human Rights Watch imedai kwamba walinzi wa pori waliwapiga baadhi ya watu wa jamii hiyo bila kujali sheria, huku wanajamii wakieleza jinsi walivyolengwa, na pia kuorodhesha madai ya visa 13 vya kupigwa kati ya Septemba 2022 na Julai 2023.

Human Rights Watch imesema mvutano wa muda mrefu kati ya mamlaka na jamii ya wafugaji wakati mwingine umesababisha mapigano makali, baada ya serikali mnamo mwaka 2022, kuanzisha mpango wa kuwahamisha takriban watu 82,000 kutoka eneo maarufu duniani la Hifadhi ya Ngorongoro na kuwapeleka wilayani Handeni, takriban umbali wa kilomita 600 kufikia mwaka 2027.

Ripoti: HRW yailaumu Tanzania kwa kuikuka haki za Wamaasai

Shirika hilo la haki pia limesema liliwahoji takriban watu 100 kati ya mwezi Agosti mwaka 2022 na Desemba 2023 pamoja na wanajamii ambao tayari walikuwa wamehamishiwa kijiji cha Msomera huko Handeni na wengine wanaosubiri kuhamishwa.