HRW yahimiza uchunguzi juu ya matukio ya kinyama Abidjan
27 Julai 2024Human Rights Watch imesema video ya sekunde 81 iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, inaonyesha wanaume 18 waliovalia sare ya kijeshi huku wengine wawili wakiuchanja mwili wa mtu kwa visu.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu kupitia taarifa limetoa mwito kwa mamlaka nchini Burkina Faso kuchunguza tukio hilo na kuwachukulia hatua kali wanajeshi wote waliohusika na unyama huo.
Soma pia: Burkina Faso yafungia mashirika zaidi ya habari ya kimataifa
Uongozi wa jeshi umeeleza mapema wiki hii kuwa unalaani vikali vitendo vya kinyama ambavyo ni kinyume na maadili ya jeshi. Jeshi hilo limeongeza kuwa linachunguza chanzo cha video hiyo kwani haionyeshi sehemu na tarehe iliyochukuliwa au utambulisho wa wahusika.
Mnamo mwezi Aprili, Human Rights Watch ililishtumu jeshi la Burkina Faso kwa mauaji ya watu 233, wakiwemo watoto 56 kaskazini mwa nchi hiyo.