1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW yawataka wabunge wa Gambia kutoruhusu ukeketaji

19 Aprili 2024

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetowa mwito kwa wabunge wa Gambia kuupinga muswaada wa kutaka kubatilishwa kwa sheria ya kupiga marufuku ukeketaji wa wanawake na wasichana nchini humo.

https://p.dw.com/p/4ezTW
Ukeketaji ulipigwa marufuku nchini Gambia lakini sasa kuna juhudi ya kuurejesha.
Ukeketaji ulipigwa marufuku nchini Gambia lakini sasa kuna juhudi ya kuurejesha.Picha: Brian Inganga/AP/picture alliance

Shirika hilo la kimataifa limesema muswaada huo unasababisha mashaka makubwa katika suala la haki za wanawake.

Ukeketaji ni kitendo kilichopigwa marufuku kisheria katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi tangu mwaka 2015, lakini mnamo mwezi March wabunge walipiga kura ya kuupeleka muswaada huo wenye utata kwenye kamati maalum ya kuutathmini kabla ya bunge kuchukua hatua ya mwisho ya kuupigia kura.

Soma zaidi: Kenya: Kampeni ya kukabiliana na ukeketaji wazinduliwa

Shirika la Human Rights Watch limesema, ikiwa bunge litaidhinisha muswaada huo uliofanyiwa marekebisho mwezi Juni, basi Gambia itakuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu tena ukeketaji.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW