1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huenda Biden akakutana na Xi Jinping

29 Agosti 2024

Rais wa Marekani, Joe Biden huenda akakutana tena na rais mwenzake wa China, Xi Jinping, pengine katika mkutano wa kimataifa mwezi Novemba.

https://p.dw.com/p/4k3o5
USA Woodside | Joe Biden und Xi Jinping
Picha: Doug Mills/AP/picture alliance

Hayo yameelezwa leo na Mshauri wa Usalama wa Marekani, Juke Sullivan baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini China.

Sullivan amesema Biden na Xi wanaweza kuhudhuria mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki, APEC utakaofanyika Peru na mkutano wa kundi la nchi 20 tajiri kiviwanda na zinazoinukia kiuchumi duniani, G20 utakaofanyika Brazil.

Akiwa China, Sullivan amekutana na Rais Xi, afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la China, Jenerali Zhang Youxia, na Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China.

Ameyaelezea mazungumzo yake na Zhang kama yenye ''manufaa sana'' na yameziruhusu pande zote mbili fursa ya kueleza kile wanachokifanya.