MigogoroUrusi
Hujuma za Urusi zaendelea kuutikisa mji wa Kharkiv
13 Mei 2024Matangazo
Hayo ni kwa mujibu wa gavana wa eneo la Kharkiv upande wa Ukraine Oleh Synie-ghubov. Gavana huyo amesema "hali ni ngumu".
Wanajeshi wa urusi waliingia Ukraine karibu na mji Kharkiv, na kuanzisha mapambano mapya katika upande wa kaskazini mashariki. Vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vya karibu miaka miwili sasa, vimekuwa kwa kiasi kikubwa vikifanyika katika upande wa mashariki na kusini.
Siku ya Jumapili Urusi ilidai kuteka vijiji tisa katika mkoa wa Kharkiv na leo Jumatatu imedai kuwa wanajeshi wake wamechukua udhibiti zaidi na kusababisha hasara kwa vikosi vya ulinzi wa eneo hilo.