1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Human Rights Watch yalaani matumizi ya silaha nzito Sudan

4 Mei 2023

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, limelaani matumizi ya silaha nzito katika maeneo yenye wakaazi wengi nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4QuY2
Vita nchini Sudan | Moshi ukifuka baada ya shambulizi mjini Khartoum
Matumizi ya silaha nzito yameshuhudiwa katika mapigano nchini SudanPicha: MOHAMED NURELDIN ABDALLAH/REUTERS

Kwenye ripoti yake iliyotolewa leo Alhamisi, Mohamed Osman, mtaalamu wa shirika hilo nchini Sudan amesema kwa kutumia zana nzito katika maeneo ya raia, pande zote za kivita zinazohasimiana Sudan zinaonesha kutojali maisha ya watu.

Shirika hilo limelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhakikisha usalama wa raia na kuwawajibisha wale wanaohusika na mgogoro huo.

Kando na hayo ni kwamba mapigano makali yameshuhudiwa mapema leo katikati ya mji mkuu Khartoum huku kila upande ukionekana kutaka kuchukua udhibiti wa mji mkuu.

Umoja wa Mataifa unawashinikiza majenerali wanaohasimiana nchini humo kuhakikisha usalama kwa misafara ya magari ya misaada ya kiutu.