ICC kuanzisha tena uchunguzi wa uhalifu Kongo
15 Oktoba 2024Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC Karim Khan amesema ataanzisha upya uchunguzi wa madai ya uhalifu uliofanyika tangu mwaka 2022, katika jimbo linalokumbwa na migogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Khan alisema ghasia za hivi karibuni katika jimbo la Kivu ya Kaskazini zinahusiana na mifumo ya vurugu na uhasama ambao umelikumba eneo hilo tangu katikati ya mwaka 2002.
oma pia:ICC's Khan calls for 'new way' to tackle DR Congo war crimes
Amesema matokeo yake madai ya hivi karibuni zaidi yanaangukia katika uchunguzi unaoendelea.
ICC ilianzisha uchunguzi kwa mara ya kwanza nchini Kongo miaka 20 iliyopita, kufuatia miaka mingi ya vita vya makundi ya wapiganaji wenye silaha.
Mwaka uliopita, serikali ya Kongo iliiomba ICC kuchunguza madai ya uhalifu huko Kivu ya Kaskazini uliofanywa na makundi yenye silaha yanayoendesha shughuli zake tangu Januari 1, 2022.