1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi kubwa yaathirika kwa COVID-19 India

29 Julai 2020

Zaidi ya nusu ya wakazi katika maeneo ya mabanda katika wilaya zenye idadi kubwa ya watu katika jiji la Mumbai nchini India wana maambukizi ya virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3g6ot
Indien Mumbai | Coronakrise
Picha: Imago Images/ZUMA Wire/A. Vaishnav

Utafiti mpya uliotolewa leo hii, ambao ulihusisha uchukuaji wa vinasaba vya kinga mwili kwa karibu watu 7,000 katika wilaya tatu za jiji la Mumbai unaonesha zaidi ya asilimia 57, miongoni mwa kundi hilo wana virusi vya corona. Lakini wakazi katika maeneo ya kawaida yasiyo ya mabanda wamebainika kuwa na asilimia 16 ya maambukizi.

Jiji hilo, ambalo ndilo kitovu cha kibiashara nchini India limeibuka kuwa kitovu cha maambukizi ya virusi, kwa kuwa na maambukizi 110,00 huku vifo vikifikia 6,184. Takwimu rasmi zinaonesha kwa jiji la Mumbani lenye jumla ya watu milioni 12.5, takribani milioni 1.5 wanaishi katika maeneo yaliyofanyiwa utafiti huo.

Ishara njema ya kupatikana kwa chanjo ya COVID-19

Indien Mumbai | Coronakrise
Watoa huduma za afya ya afya mjini MumbaiPicha: Imago Images/Hindustan Times

Na katika hatua nyingine ya faraja, Waziri wa Utafiti wa Ujerumani Anja Karliczek amesema kuna ishara ya uwezekano wa kupatikana kwa kinga ya virusi vya corona kabla ya katikati ya mwaka ujao. Akizungumza na waandishi wa habari waziri huyo alisema bado wanaendelea kuwa na makidirio ya kwamba kinga hiyo itaweza kupatikana tu, katika kipindi hicho cha mwaka.

Wakati kukitajwa matumaani hayo kwa Ujerumani pia, kunaonekana kupatikana kwa nuru ya uchumi, ambapo sasa inaelezwa unakua kwa asilimia 3 katika kipindi hiki, baada ya hapo awali kuvurugwa na janga la virusi vya corona. Taasisi ya Uchumi ya DIW kwa hatua hiyo ni wazi kwamba hali inaendelea kuwa na unafuu na itachukua takribani miaka miwili ili kuondosha kabisa athari za janga hilo.

Uhispania uvaaji wa barakoa ni lazima

Serikali ya Uhispania imeamuru uvaaji wa barakoa katika maeneo ya umma kuwa jambo la lazima. Lengo ni kudhibiti maambukizi kwa makundi ya watu ambayo yanakutana katika maeneo ya wazi kwa wakati mmoja. Pamoja na hatua hiyo bado kanuni za afya zinazuia watu wasikutane zaidi ya 10 katika eneo moja. Huko Marekani bado hali si nzuri wasafiri katika kutoka katika majimbo 34, pamoja na Puerto Rico na Columbia lazima wakae wawekwe karantini kama walifanya safari za  New York, New Jersey na Connecticut.

Soma zaidi:COVID-19- Vifo vyapindukia 600,000 ulimwenguni kote

Na Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya uratibu wa misaada ya kiutu imetoa kiasi cha dola milioni 100 cha dharura kwa ajili ya kusaidia mataifa 10 kwa utaratibu maalumu ambayo yameathirika sana na virusi vya corona huko Afrika, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kusini na Kaskazini. Kiasi hicho kinafanya kufikiwa jumla jumla ya dola milioni 225 ambacho kilitolewa kusaidia mataifa 20 kwa mwaka huu.

Chanzo: RTR, DPAE, APE,