1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko Kenya yapanda hadi 120

29 Novemba 2023

Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Raymond Omollo amesema watu kutoka takribani kaya 90,000 wameyakimbia makaazi yao na wamepewa hifadhi ya muda katika kambi 120.

https://p.dw.com/p/4ZZRC
Kenya Mombasa 2023 | Mafuriko
Maeneo ya pwani ya Kenya yamekumbwa na mafuriko yaliosababisha vifo vya watu 120.Picha: REUTERS

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Kenya imepanda hadi karibu watu 120. Waziri wa mambo ya ndani Raymond Omollo amesema watu kutoka takribani kaya 90,000 wameyakimbia makaazi yao na wamepewa hifadhi ya muda katika kambi 120.

Hakutoa taarifa zozote kuhusu jumla ya idadi ya watu walioathirika na mafuriko hayo ya wiki kadhaa. Serikali imesema Kaunti 38 kati ya 47 za nchini humo zimeathirika na mvua hiyo ambayo imesababisha pia maporomoko ya tope.

Soma pia: Rais Ruto atangaza mikakati ya kukabiliana na mafuriko

Mafuruko hayo yametokana na mvua kubwa inayonyesha ya El Nino. Mvua kubwa pia imekuwa ikinyesha katika nchi jirani ya Somalia. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, vifo vingi vimeripotiwa na idadi kubwa ya watu wamevikimbia vijiji na miji yao kutokana na mafuruko.