1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Idadi ya watu kufikia bil.8 ifikapo Novemba

Hawa Bihoga
11 Julai 2022

Makadirio ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya watu ulimwenguni yanaonesha kwamba hadi kufikia mwezi Novemba idadi ya watu inatarajiwa kufikia bilioni 8 duniani,huku India ikitajwa kuipuki China ifikapo 2023.

https://p.dw.com/p/4DyWR
NUR FÜR DW AKADEMIE | Indien Kolkata homeless
Picha: Andrea Zangrilli/Travel Wild/stock.adobe.com

 Hadi sasa nchi zote mbili India na China zina idadi sawa ya watu bilioni 1.4, lakini kulingana na ongezeko la vizazi nchini India huenda likaipiku China kufikia mwaka 2023.

Idadi ya watu inakadiriwa kuwa bilioni 8 kufikia Novemba 15 mwaka huu na inaweza kufika bilioni 8.5 ifikapo mwaka 2030, bilioni 10.4 kwa mwaka 2100, kutokana na kupungua kwa kasi ya idadi ya vifo, ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliotolewa siku ya Jumatatu imesema.

Idadi ya watu India ilikuwa bilioni 1.21 mwaka 2011, kwa mujibu wa sensa ya taifa hilo ambayo hufanyika mara moja katika muongo mmoja, serikali ya taifa hilo ilihairisha sensa ya mwaka 2021 kutokana na hjanga la Covid-19.

Soma pia:Utumiaji holela wa vidonge vya uzazi vya P2 kwa wasichana na hatari inayowakabili

Idadi ya watu duniani imetajwa kuongezeka kwa kiwango kidogo sana mwaka 2020 ambapo iliongezeka kwa asilimia moja tu tangu mwaka 1950.

Hali ya vizazi yaporomoka duniani

katika mwaka 2021 wastani wa uzazi kwa idadi ya watu duniani ulikuwa ni vizazi 2.3 kwa mwanamke ambapo kiwango kimeshuka kutoka vizazi 5 mwaka 1950. Uzazi kwa ujumla duniani unatazamiwa kushuka hadi kufikia vizazi 2.1 kwa mwanamke mmoja kufikia mwaka 2050.

Tansania Frühgeborene
Mguu wa mtoto mchangaPicha: DW/H. Bihoga

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema hii ni sababu ya kusherehekea utoafauti wetu, kutambua ubinadamu wetu wa pamoja na maajabu ya maendeleo ya afya ambayo yameongeza umri wa kuishi na kupunguza kiwango cha vifo vya wajawazito na watoto.

Amesema "bado kuongezeka kwa idadi ya watu duniani ni ukumbusho wa wajibu wetu kwa pamoja kuiangalia dunia na kujitathimini pale tuliposhindwa kutekeleza majukumu yetu" Alisema Guterres.

Soma pia:2020: Miaka 60 tangu kuzinduliwa vidonge vya kuzuia ujauzito

Kufuatia ripoti ya awali ya shirika la afya ulimwenguni WHO ambayo ilikadiria vifo milioni 14.9 vilivyotokana na janga la Corona kati ya Januari 2020 na Desemba 2021, ilionesha kiwango cha  miaka ya kuishi kwa ujumla imeshuka kufikia miaka 71 mwaka 2021 kutoka miaka 72.8 mwaka 2019, haswa kutokana na janga la Corona.

Tanzania miongoni mwa mataifa yatayokuwa na idadi kubwa ya watu

Umoja wa mataifa umesema kwamba zaidi ya nusu ya ongezeko la idadi ya watu linalotazamiwa kutokea hadi mwaka 2050 litakuwa zaidi katika nchi 8, ambazo ni Congo, Misri, Ethiopia, India, Nigeria, Pakistan, Ufilipino pamoja na Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Soma pia:UNFPA-Mamilioni ya wanawake na wasichana hawana maamuzi na miili yao

Mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara yanatazamiwa kuchangia zaidi ya nusu ya ongezeko hilo linalotarajiwa  kwa mwaka 2050. Hata hivyo idadi ya watu kati ya mataifa 61 inakadiriwa kupungua kwa asilimia 1 au zaidi kati ya mwaka 2022 na 2050 kunakosababishwa kushuka kwa uzazi.

COVID yapaisha matumizi ya nji za uzazi wa mpango