1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Idara ya Usalama nchini Marekani yachunguzwa tena

17 Septemba 2024

Idara ya Usalama nchini Marekani ilikabiliwa na uchunguzi mpya jana Jumatatu baada ya jaribio la pili la mauaji dhidi ya mgombea wa urais Donald Trump, katika kipindi cha miezi miwili.

https://p.dw.com/p/4khB8
Marekani Butler Trump
Wana usalama wa taifa wenye jukumu la kulinda viongozi wakimuondoa mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump baada ya kushambuliwa kwenye mkutano wa hadhara, Julai 13, 2024Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Idara hiyo imekuwa ikiyumba tangu shambulizi la Julai 13 dhidi ya Trump kwenye mkutano wa kampeni huko Pennysylvania, na kusababisha Mkurugenzi wa idara hiyo Kimberly Cheatle kujiuzulu na kukiri kwamba walishindwa kiulinzi.

Maafisa watano wa idara hiyo pia wako likizo wakisubiri uchunguzi kukamilika kuhusiana na kudororora kwa usalama.

Rais Joe Biden alipozungumzia shambulizi hili la karibuni alisema idara hiyo inayotakiwa kuwalinda viongozi wa ngazi za juu inahitaji msaada zaidi.