1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IDEA: Demokrasia ya dunia yaendelea kuporomoka

Josephat Charo
17 Septemba 2024

Idadi ndogo ya wapiga kura wanaojitokeza kupiga kura na kesi zinazoongezeka za matokeo ya uchaguzi kuzozaniwa ni mambo yanayotishia uhalali wa chaguzi na demokrasia.

https://p.dw.com/p/4kiIv
Dar es Salaam, Tanzania | Afrika | Demokrasia | Mwanamke akikamilisha upigaji kura.
Mwanamke akikamilisha zoezi la kupiga kura nchini Tanzania.Picha: Emmanuel Herman/REUTERS

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyochapishwa hivi leo na shirikia la kimataifa lisilo la kiserikali lenye makao yake mjini Stockholm nchini Sweden.

Taasisi ya kimataifa ya Demokrasia na msaada wa masuala ya uchaguzi IDEA imesema mwaka 2023 ulikuwa wa nane mfululizo kuwa na kunywea kwa demokrasia, kipindi ambacho kinaelezwa kuwa ni kirefu mfululizo cha anguko la demokrasia tangu rekodi zilipoanza kuwekwa mnamo 1975.

Soma pia:Taasisi ya demokrasia ya Sweden yasema demokrasia imashakani kote duniani

Katibu Mkuu wa IDEA Kevin Casas-Zamona amesema ripoti hii ni wito wa kuchukua hatua kulinda chaguzi za kidemokrasia. Pia amesema mafanikio ya demokrasia yanategemea mambo mengi, lakini inakuwa haiwezekani kama chaguzi zinafeli.