Tume ya kukabiliana na ufisadi nchini Kenya, EACC, imegeukia kutafuta ushawishi wa viongozi wa kidini baada ya tume ya uchaguzi nchini humo IEBC kuwaidhinisha viongozi ambao uadilifu wao unatiliwa shaka. EACC imeonya kuwa bunge lijalo huenda likawa na viongozi wengi wenye maadili ya kutiliwa shaka na wanaohusishwa na ufisadi. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Wakio Mbogho kutoka Nakuru.