Wagombea wote wanne wa urais wanajiandaa kukutana na tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC ili kujadili suala la fomu za kuandaa matokeo ya uchaguzi. Wakati huo huo, IEBC imeweka bayana kuwa sakata la vibandiko vya uchaguzi vilivyoingizwa nchini katika mazingira ya kutatanisha limesuluhishwa. Sikiliza ripoti ya Thelma Mwadzaya kutoka Nairobi.