1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF yafikiria kuongeza msaada wake kwa Ugiriki

28 Aprili 2010

Shirika la Fedha la Kimataifa IMF linafikiria kuongeza mchango wake kwa euro bilioni 10 katika mpango wa kuisaidia Ugiriki iliyokumbwa na matatizo makubwa ya deni.

https://p.dw.com/p/N8Wm
t.European Central Bank President Jean-Claude Trichet, left, talks with Greece's Finance Minister Giorgos Papaconstantinou, right, prior to the Eurogroup meeting at the European Union Council building in Brussels, Monday Feb. 15, 2010. (AP Photo/Thierry Charlier)
Waziri wa Fedha wa Ugiriki, George Papaconstantino(kulia) na Rais wa Benki Kuu ya Ulaya, Jean-Claude Trichet.Picha: AP

Ugiriki imepangiwa msaada wa euro bilioni 45 na hadi sasa IMF imekubali kutoa theluthi moja ya pesa hizo na nyingine zitatoka nchi za kanda inayotumia sarafu ya euro katika Umoja wa Ulaya. Lakini kwa mujibu wa mchambuzi alienukuliwa na gazeti la Financial Times, IMF ipo tayari kuongeza mchango wake hadi euro bilioni 25 na suala hilo linajadiliwa na wahusika. Fedha hizo zinaweza kutolewa kama mkopo wa miaka mitatu aliongezea mchambuzi huyo alie karibu na majadiliano yanayofanywa mjini Athens.

Hata waziri wa Fedha wa Canada Jim Flaherty hivi karibuni alisema kuwa Ugiriki itahitaji msaada mkubwa zaidi ya ule uliopangwa hapo awali lakini hakutaka kueleza juu ya kiwango kinachojadiliwa. Nae Waziri wa Fedha wa Ugiriki George Papaconstantinou alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo msaada huo utafikia euro bilioni 80 hadi 90, alisema hawezi kutaja ni kiasi gani lakini ameridhika na majadiliano yanayofanywa pamoja na IMF na Umoja wa Ulaya.Lakini hapo hapo akaulaumu Umoja wa Ulaya kuwa unachelewesha msaada. Akaonya kuwa Ugiriki inapaswa kulipa deni la euro bilioni 9 ifikapo Mei 19.

Siku hiyo ikijongolea, Rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy ameitisha mkutano wa dharura wa viongozi wa kanda ya euro, kujadili njia ya kuisaidia Ugiriki. Mkutano huo unatazamiwa kufanywa mjini Brussels tarehe 10 Mei. Ujerumani ambayo hapo awali ilikuwa ikisitasita kuhusu msaada huo, sasa imeashiria kuwa ipo tayari kuutekeleza mpango wa kuinusuru Ugiriki.

ARCHIV - Bundesfinanzminister Wolfgang Schaeuble spricht am 10. Dezember 2009, in Berlin auf einer Pressekonferenz nach der Sitzung des Finanzplanungsrates. Der Kauf der brisanten CD mit den Daten von 1.500 deutschen Steuersuendern durch den Fiskus ist so gut wie beschlossen. "Im Prinzip ist die Entscheidung gefallen", sagte Finanzminister Wolfgang Schaeuble der "Augsburger Allgemeinen" am Dienstag, 2. Februar 2010 (Mittwochausgabe). (AP Photo/Gero Breloer) ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- FILE - German Finance Minister Wolfgang Schaeuble talks during a news conference in Berlin, Dec. 10, 2009. Panel in the background reads finances. (AP Photo/Gero Breloer)
Waziri wa Fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schaeuble.Picha: AP

Kwani Waziri wa Fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schäuble katika mahojiano yake na gazeti la Handelsblatt amesema mpango huo unahitaji kukamilishwa na kutekelezwa, ili kutuma ujumbe waziwazi kuwa Ugiriki haitoachiwa peke yake. Ujerumani ndio itakayolipa sehemu kubwa ya msaada utakaotolewa na nchi za kanda ya Euro.

Mchango wa Ujerumani ukiwa ni kama euro bilioni 8.4 wananchi wake wanapinga kabisa kuisaidia Ugiriki na sasa suala hilo limekuwa mada tete ya kisiasa kwa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, hasa chama chake cha CDU kikitetea madaraka yake katika uchaguzi utakaofanywa tarehe 9 Mei katika jimbo la North Rhine Westphalia.

Mwandishi: P.Martin/RTRE/AFP

Mhariri: Mwadzaya,Thelma