1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Khan ahukumiwa kifungo cha miaka 14 jela kwa ufisadi

31 Januari 2024

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan pamoja na mkewe wamehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela kwa madai ya ufisadi.

https://p.dw.com/p/4btUl
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran KhanPicha: Aamir Qureshi/AFP/Getty Images

Hukumu hii inatolewa siku moja baada ya mahakama nyingine maalumu kumuhukumu Khan kwa kuvujisha siri za serikali na kumuhukumu kifungo miaka 10 jela.

Hukumu hii ya leo, ni ya kesi ya karibuni zaidi ya ufisadi ya kuuza na kubaki na zawadi za serikali wakati akiwa madarakani.  

Hata hivyo, mwanasheria wake, Chaudhary Zaheer Abbas, amesema wataikatia rufaa hukumu hii.

Abbas amesema, "Hakuna tofauti katika hukumu zote hizi mbili kwa sababu ni sehemu ya ajenda na mpango wa mtu aliyefanya hivyo. Na hata ingekuwa vinginevyo, hukumu hii ilikuwa ya upendeleo, hakukua na mashauriano, wala fursa ya ushahidi."

Hii ni hukumu ya tatu tangu mwaka 2022, wakati Khan alipoondolewa madarakani na atatumikia vifungo vyote vitatu kwa pamoja.