1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

India, China na Brazil zaweza kuwa wapatanishi, asema Putin

5 Septemba 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema China, India na Brazil zinaweza kuwa wasuluhishi endapo mazungumzo ya kuleta amani yatafanyika juu ya vita vya Urusi na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4kIiS
Rais wa urusi Vladimir Putin (kushoto) na makamu wa rais wa China Han Zheng
Rais wa urusi Vladimir Putin (kushoto) na makamu wa rais wa China Han ZhengPicha: AFP

Putin ameyasema hayo kwenye mkutano wa kiuchumi wa nchi za kanda ya ulaya Ulaya mashariki na bara la Asia unaofanyika katika mji wa Vladivostok, ulio takriban kilomita 45 kutoka kwenye mpaka wa na Urusi na China.

Amesema makubaliano ya awali yaliyofikiwa kati ya wajumbe wa Urusi na Ukraine nchini Uturuki ambayo hayakutekelezwa, yanaweza kuwa msingi wa mazungumzo mapya.

Wajumbe wa Urusi na Ukraine walikutana kwa ajili ya mazungumzo hayo ya awali mjini Istanbul, mnamo wiki za kwanza baada ya vita kufumuka mwaka 2022.