India na China zimekubaliana kutuliza machafuko ya mpakani
18 Juni 2020Matangazo
Makubaliano hayo yameafikiwa licha ya pande hizo mbili kutupiana lawama kuhusu makabiliano yaliyosababisha vifo vya wanajeshi 20 wa India. Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili Wang Yi na Subrahmanyam Jaishankar, walizungumza kwa njia ya simu kutuliza taharuki, baada ya makabiliano hayo ya ngumi, mikwaju na marungu. Hata hivyo, duru zimeliarifu shirika la habari la AFP kwamba mazungumzo hayo yamefanyika mnamo wakati India inawapeleka maafisa wake wa kukabiliana na fujo katika eneo hilo Himalaya nyuma ya Tubet. Wakati huo huo, kituo cha televisheni kinacvhomilikiwa na serikali ya China CCTV, kimeonyesha kanda ya video ya majeshi ya China yakifanya luteka katika eneo la Tibet.
Chanzo: AFPE