India na Israel kuimarisha uhusiano
5 Julai 2017Waziri Mkuu wa India Narendra Nodi leo amekuwa na mazungumzo na mwenzake wa Israel, Banjamin Netanyahu, wakati viongozi hao wakiwa katika juhudi za kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili kupindukia mikataba ya gharama kubwa ya shughuli za ulinzi.
Viongozi hao wamewasilisha maikataba kadhaa kati ya India na Israel ya ushirikiano kwa teknolojia ya satalaiti, maji na kilimo halikadhalika kuanzishwa kwa mfuko wa ubinifu wa dola milioni 40.
Mikataba hiyo ni sehemu ya juhudi za kutanuwa uhusiano katika fani ya kiraia kati ya nchi hizo mbili wakati Israel tayari ikuuzia India wastani wa zana za kijeshi unaofikia thamani ya dola bilioni moja kwa mwaka.
Netanyahu na Modi wamekuwa wakisalimiana kwa furaha wakati wa ziara yote hiyo ya siku tatu ambayo imeanza jana Jumanne na kuita ziara hiyo kuwa ya kihistoria.
Netanyahu kufuatia mazungumzo yake na Modi mjini Jerusalem amesema na hapa nanukuu: "Nahisi leo hii India na Isarel zimekuwa zikibadilililishana ulimengu wote na yumkini kubadili sehemu ya dunia." Mwisho wa kunukuu.
Kutanuwa ushirikiano
Ameongeza kusema wamewataka wafanyakazi wao kuanzisha mipango madhuhuti ya kuendeleza ushurikiano zaidi katika fani mbalimbali kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Modi amesema mazungumzo yao yamepindukia suala la miradi baina ya nchi hizo mbili na kuangalia vipi ushirikiano wao unaweza kusaidia amani na utengamano duniani.
Waziri Mkuu huyo wa India pia amesema wamekubaliana kushirikiana kwa mengi ili kulinda maslahi yao ya kimkakati na pia kushirikiana kupambana na kuongezeka kwa itikadi kali na ugaidi pamoja na usalama wa mtandaoni.
Netanyahu na mafisa wengine wa serikali walimkaribisa waziri mkuu kwa heshima ya kutandikiwa zulia jekundu wakati alipowasii katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion mjini Telv Aviv kuanza ziara yake ya nchini Israel hapo jana ambapo alikaribishwa na Rais Rueven Rivlin katika kasri lake mjini Jerusalem na kuwa na mawili matatu ya kizungumza:
Modi amesema :"Mheshimiwa katika maneno yako ya utambulisho umetumia misemo inayotumika katika ulimwengu wa biashara kwamba ni G2G serikali kwa serikali na BG2 biashara kwa serikali lakini katika dunia halisi namaanisha leo hii tunaona jicho kwa jicho lakini ninavyosema hivyo simaanishi ule usemi mashuhuri naamanisha kwamba India ni kwa ajili ya Israel na Israel kwa ajili ya India."
Miaka 25 ya uhusiano wa kidiplomasia
Ziara hiyo ya Modi nchini Israel inaadhimisha miaka 25 tokea India na Israel zilipoanzisha uhusiano wake wa kidilplomasia.
Israel imekuwa inayotafuta washirika katika Umoja wa Mataifa na washirika wapya kibiashara imeelezea ziara hiyo kama ni ushindi mkubwa wa kidiplomasia.
Wachambuzi wa Israel wamesema Modi hatarajiwi kwenda Ramallah kukutana na viongozi wa Kipalestina wakati wa ziara yake hiyo ya siku tatu jambo ambalo ni la kawaida kwa wageni wanaoitembelea Israel kutoka mataifa ya kigeni.
Mwandishi: Mohamed Dahman/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef