India yapendekeza matumizi ya chanjo ya nyumbani
12 Oktoba 2021Nchini Ujerumani wizara ya afya imeripoti kuwa asilimia 10 ya wagonjwa waliotibiwa dhidi ya virusi vya Corona katika vyumba vya wagonjwa mahututi kati ya Agosti na Septemba walikuwa wamepata chanjo kamili. Soma HRW: Misaada ya Covid-19 Afrika haikuwafikia walengwa
Kulingana na data za serikali India kufikia sasa imefanikiwa kutoa chanjo kwa karibu asilimia 29 ya watu takribani milioni 944, wenye sifa za kuchanjwa kulingana na data za serikali, ikiwemo utoaji wa dozi zaidi ya milioni 110 za chanjo ya nyumbani ya Covaxin inayotengenezwa na kampuni ya Bharat Biotech. soma Wimbi la maambukizi ya Covid-19 bado laitikisa India
Kampuni hiyo hata hivyo, bado iko katika mchakato wa kupata ruhusa ya kuorodheshwa kwa chanjo yake na shirika la afya duniani WHO, ili itolewe kwa matumizi ya dharura, uamuzi ambao unatarajiwa kutolewa baadaye mwezi huu. soma Ulaya kuongeza chanjo milioni 200 za corona Afrika
Nchi kadhaa zimekuwa zikifanya kazi kuidhinisha chanjo kwa watoto, huku Marekani ikipitisha chanjo ya Pfizer kuwa salama kwa watoto wenye umri wa miaka 12 na zaidi.
Hata hivyo Bodi ya Kudhibiti Dawa pamoja na Kamati ya Wataalam nchni India imetoa mapendekezo chanya juu ya utumiaji wa chanjo hiyo ya nyumbani kwa watoto kati ya umri wa miaka 2-18.
Nchini Ujerumani
Huku haya yakiarifika taarifa iliyotolewa na wizara ya Afya nchini Ujerumani imesema mgonjwa mmoja kati ya 10 waliotibiwa dhidi ya virusi vya Corona katika vitengo vya wagonjwa mahututi nchini humo kuanzia mnamo Agosti na Septemba walikuwa wamepewa chanjo kamili.
Kulingana na ripoti hiyo, jumla ya wagonjwa 11,419 wa Corona walitibiwa katika kitengo cha wangonjwa mahututi kati ya Februari na katikati mwa Septemba. Kati yao, 210 walikisiwa kuwa walipokea chanjo.
Barani Afrika Rwanda, Senegal na Afrika Kusini zimetajwa kama mataifa yanayoweza kuwa wenyeji wa kiwanda cha chanjo ya Moderna kinachopangwa kujengwa barani Afrika. Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti na mwanzilishi mwenza wa kampuni hiyo ya dawa wakati ikiongeza juhudi za kufatuta eneo la kujenga kiwanda hicho barani.
Afrika
Wataalam wa afya wamesema Rwanda, Senegal na Afrika Kusini zimetajwa katika orodha hiyo kwa sababu yumkini zina utaalamu wa kutengeneza na kuzalisha chanjo, au zimeonyesha nia ya kuendeleza tasnia hiyo.
Kampuni ya Moderna siku ya Ijumaa ilisema kwamba inalenga kutoa dozi bilioni 1 za chanjo ya COVID-19 kwa nchi zenye kipato cha chini kufikia 2022, mbali na dozi ambao tayari imejitolea katika mpango wa ulimwengu wa kushiriki chanjo COVAX.
Vyanzo: Reuters/dpa