India yashambulia katika ardhi ya Pakistan
26 Februari 2019Ndege za kijeshi za Pakistan zimeshambulia kambi ya wanamgambo katika ardhi ya Pakistan hii leo. Waziri wa mambo ya nje wa India na duru za serikali zimesema wanamgambo 300 wameuwawa katika tukio hilo,ingawa Paskitan ambayo imeingia katika mgogoro mkubwa na India kuhusiana na suala hilo imekanusha juu ya kuwepo wahanga wowote.
Mivutano kati ya India na Pakistan ilianza kuongezeka Februari 14 baada ya kutokea mashambulio ya kujitowa muhanga katika jimbo la Kashmir upande wa India. Jumanne (26.02.2019) India imesema ndege zake zimeshambulia upande wa Pakistan na kulenga kambi ya mafunzo ya wanamgambo wa Jaesh e Mohammed Jem,kundi ambalo lilidai kuhusika na shambulizi la bomu la kutegwa ndani ya gari lililofanywa na mshambuliaji wa kujitoa muhanga ambalo lilisababisha kuuwawa kiasi askari wa India wa kikosi maalum katika jimbo la Kashmir.
India imesema imeamrisha mashambulio hayo dhidi ya ardhi ya Pakistan asubuhi ya leo kutokana na taarifa zao za kijasusi zinazosema kwamba kundi la Jaesh lilikuwa likiandaa mashambulizi mengine zaifdi dhidi ya India.Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa India Vijay Gokhale amewaambia waandishi habari kwamba kutokana na hatari iliyokuwepo,ilikuwa ni muhimu kufanyika mashambulizi hayo.
Mwanadiplomasia huyo pia ameinyooshea kidole moja kwa moja Pakistan kushirikiana na wanamgambo wa Jem akisema kuwepo kwa kambi ya mafunzo kama hiyo yenye uwezo wa kutoa mafunzo kwa mamia ya wapiganaji wa Jihadi hakungeweza kufanikiwa bila ya ufahamu wa maafisa wa serikali ya Pakistan.
Hata hivyo Pakistan inakanusha kuwahifadhi wanamgambo wa JeM,kundi ambalo kimsingi linaipinga India na linamafungamano na mtandao wa kigaidi wa Alqaeda na tangu mwaka 2001 limejumuisha kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa ya magaidi.Ikumbukwe kwamba kundi hili liliwahi kufanya mashambulio makubwa dhidi ya bunge la India Desemba 2001 likishirikiana na wanachama wa kundi jingine la wanamgambo lililoko Pakistan linalojiita Lashkar-e- Taiba.Rais wa Pakistan Arif Alvi amesema India imesababisha hisia zisizoweza kudhibitiwa tangu lilipotokea shambulio dhidi ya wanajeshi wake katika jimbo lenye kuzozaniwa la Kashmir..
Katika kanda hii au kwingine kokote,pamoja na kufahamu kwamba wanaweza kuidhuru nchi yangu,tunajua sisi ni watu tunaolindwa na vikosi vyetu na tunajua jinsi ya kuilinda nchi yetu.Hatuna nia mbaya kwa nchi yoyote ile,lakini tunajua jinsi ya kujilinda wenyewe,mabibi na mabwana na hivyo ndivyo tutakavyofanya.
China imezitaka Paskitan na India kujizuia na matumizi ya nguvu baada ya tukio la ushambuliaji uliofanywa na India kwenye eneo la Muzafarabad katika jimbo la Kashmir.
Mwandishi:Saumu Mwasimba
Mhariri: Sekione Kitojo