SiasaChina
Indonesia yazungumzia ushirikiano wa China amani ya Myanmar
22 Februari 2023Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Retno Marsudi, amesema anauthamini uungaji mkono wa China wenye kuzingatia mambo matano muhumu kwa ajili ya kuhitimisha utawala wa kiimla wa kijeshi nchini Myanmar.
Retno ameyazungumza hayo baada ya mkutano wake na mwenzake wa China, Qin Gang mjini Jakarta.
Myamnar imeingia katika mfululizo wa vurugu, kudorora kwa uchumi pamoja na ukosefu wa utulivu wa kisiasa tangu mapema 2021.
Mataifa yaliyo katika muungano wa ASEAN, ambayo Indonesia wakati huu inashikilia uwenyekiti wa kupokezana, yanakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na watawala wa kijeshi kutokuwa tayari kutekeleza makubaliano yaliyoridhiwa muda mfupi baada ya mapinduzi ya Februari mwaka 2021, ambayo yalisainiwa na kiongozi mkuu wa kijeshi.