1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Infantino azungumzia ushindani wa Kombe la Dunia

24 Septemba 2018

Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani – FIFA Gianni Infantino ametoa wito kwa shirikisho lake kufanya juhudi zaidi za kuyasaidia mabara ya Amerika Kusini, Afrika na Asia kushindana dhidi ya Ulaya katika Kombe la Dunia

https://p.dw.com/p/35PEh
Russland Moskau - FIFA Kongress
Picha: Reuters/S. Karpukhin

Timu za UIaya zimeshinda matamasha manne yaliyopita ya Kombe la Dunia na kuwakilishwa na timu nne katika nusu fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi 2018. "Tunapaswa kuboresha kandanda, sio tu mashindani bali pia katika ngazi ya juu kote duniani. Hiki kipanaswa kuwa kipaumbele chetu katika kusonga mbele, na hiki ndicho tunachoangazia bila shaka katika FIFA na tunachowataka nanyi mkiangazie".

Kocha wa Morocco Mfaransa Herve Renard anakiri kuwa panahitajika mpango wa utekelezaji akiongeza kuwa pengo linazidi kuwa kubwa lakini haoni kama kutanua Kombe la Dunia hadi timu 48 kimsingi ni wazo zuri. "kwa maoni yangu, nadhani 32 tayari zilikuwa timu nyingi. Bila shaka tulifurahi kwa sababu tulishiriki katika Kombe la Dunia Urusi. Naelewa umuhimu wa kutoa fursa kwa timu nyingi katika Kombe la Dunia ambalo ndio tamasha bora kabisa duniani maana unafurahi wakati timu inapoiwakilisha nchi yako. Lakini kuhusu kandanda, sina uhakika kama ni jambo zuri. Hayo ni maoni yangu

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman